Hatua 12 Za Uhakika Za Kujenga Utajiri Mkubwa Kwenye Maisha Yako.

NGUVU YA BUKU.

NGUVU YA BUKU; Jenga Utajiri Mkubwa Kwa Kuanza Na Kiasi Kidogo Cha Fedha.

Fedha ndogo ndogo zinazopita kwenye mikono yako, ambazo unaweza kuzidharau sana ndiyo zimebeba mbegu ya utajiri mkubwa unaoutaka kwenye maisha yako.

Karibu kwenye programu maalumu ya NGUVU YA BUKU. Hii ni programu ya kujifunza na kufanya uwekezaji kwa vitendo, kwa kuanza na kiasi kidogo kabisa cha fedha ambacho kila mtu mzima mwenye afya na akili timamu anaweza kukipata.

Utaratibu wa programu ya NGUVU YA BUKU ni kama ifuatavyo;

1. Hii ni programu ya wazi kwa watu wote wenye kiu ya kujenga utajiri na uhuru wa kifedha kwenye maisha yao kwa kutumia njia ambazo ni halali. Kupitia programu hii tunajenga mtazamo sahihi juu ya fedha na utajiri na kuwa na msukumo wa kujenga utajiri mkubwa kwenye maisha yetu.

2. Mshiriki wa programu lazima awe tayari kujifunza kuhusu fedha na uwekezaji na kufanyia kazi kwa vitendo hayo anayojifunza. Kwenye programu hii kujifunza na kuwekeza ni endelevu. Kila siku unajifunza na kila wiki unafanya uwekezaji bila kutoa uwekezaji huo kwa angalau miaka 10.

3. Mshiriki wa programu lazima awe na kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI ambacho ndiyo nguzo kuu ya programu ya NGUVU YA BUKU. Kila mshiriki atasoma kurasa 10 za kitabu hicho kwa siku na kushirikisha yale aliyojifunza na hatua anazoenda kuchukua. Kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI kitasomwa kwa mwendelezo.

4. Mshiriki lazima awe kwenye kundi maalumu la programu ya NGUVU YA BUKU ambapo ataendelea kupata mafunzo endelevu kuhusu fedha na uwekezaji. Kila mshiriki anapaswa kuonyesha ushirikiano wa asilimia 100 kwenye taratibu za kundi.

5. Mshiriki lazima awe na akaunti ya uwekezaji kwenye mfumo wa uwekezaji wa mifuko ya pamoja wa UTT AMIS. Kwa ambao bado hawajawa na akaunti wataelekezwa jinsi ya kufungua na kuwekeza. Kwa wenye akaunti ambazo zina malengo mengine, wanatakiwa kufungua akaunti maalumu kwa ajili ya programu hii ambayo hawatatoa fedha wanazowekeza.

6. Mshiriki anapaswa kuweka pembeni kiasi cha fedha kisichopungua elfu moja kila siku ya wiki, Jumatatu mpaka Jumapili. Kama hujui unawezaje kutenga kiasi cha Tsh 1,000/= kila siku, anza kwa kupunguza matumizi ya kiasi hicho kwenye kila siku yako. Kwenye programu utaendelea kujifunza njia za kuongeza kipato chako zaidi.

7. Kila siku ya Jumatatu, kila mshiriki anaweka UTT fedha aliyokusanya kwenye wiki nzima iliyoisha, kiasi kisichopungua elfu 7. Akishaweka kiasi hicho cha fedha anatuma risiti ya ushahidi kwenye kundi la programu ya NGUVU YA BUKU. Ushahidi unatumwa siku hiyo ya Jumatatu na washiriki wote bila kukosa.

8. Kila siku ya Ijumaa, kila mshiriki anatakiwa kutuma ushahidi wa salio la uwekezaji wake kwenye mfuko wa UTT aliouchagua kwenye hii programu. Mpango wa programu ni kuweka bila kutoa, hivyo ushahidi wa Ijumaa ni kukuzuia usiingie tamaa ya kutoa uwekezaji huo.

9. Kila mshiriki ataendelea kuongeza kiwango chake cha kuwekeza kadiri muda unavyokwenda na kipato chake kuongezeka. Kiasi kidogo cha Tsh 1,000/= ni cha chini ili kupata sifa, lakini inashauriwa kuwekeza kwa ukubwa zaidi. Muhimu ni usiwekee malengo yoyote ya matumizi kiasi unachowekeza kupitia programu huu ya NGUVU YA BUKU.

10. Kutokufuata taratibu za programu ya NGUVU YA BUKU kutapelekea uikose huduma hiyo kwa sababu utaondolewa. Ukishaondolewa kwenye programu, itakuingia gharama kubwa kuweza kurudi. Fuata utaratibu huu ili uweze kunufaika na programu ya NGUVU YA BUKU.

Karibu usikilize kipindi cha ONGEA NA KOCHA cha leo ili ujifunze kwa kina zaidi kuhusu dhana hii ya kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa kupitia kufanya kitu ulichochagua kila siku bila kuacha.

Angalia kipindi hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.utajiri.tz